Ikiwa una tatizo la afya ya akili, wasiliana nasi sasa.
Huwa tunatoa usaidizi wa haraka kwa vijana walio na tatizo.
Huwa tunatoa usaidizi wa haraka kwa vijana walio na tatizo.
Usaidizi kutoka kwa wafanyakazi wa ndani wa tatizo la afya ya akili upo masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.
Tunaweza kukutana nawe ana kwa ana na/au kuzungumza nawe kupitia simu ili kukusaidia na tatizo lako.
Ikiwa uko kwenye hatari ya moja kwa moja, piga simu kwa 911
Itikio la tatizo la afya ya akili hutolewa bila kujali uwezo wako wa kulipa.
Wafanyakazi wa tatizo la afya ya akili wapo masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki ili kutoa usaidizi na ushauri nasaha. Tunaweza kukusaidia kushinda hali ngumu na kushughulikia tatizo hilo.
Tunaweza kukusaidia kumtuliza mtu mwenye hasira, asiyeweza kudhibitika au aliyeudhika. Pia tunaweza kukusaidia kuweka hali iwe salama zaidi.
Wafanyakazi watakusaidia kuunda mpango wa kushughulikia tatizo, sasa na katika hali za siku zijazo.
Kutuliza tatizo ni huduma ya kufuatilia inayofanywa nyumbani inayoweza kudumu hadi wiki nne.
Timu yetu hufanya kazi na mashirika ya jamii, hospitali, shule, na watekelezaji sheria ili kusaidia kuelewa afya ya akili vyema zaidi.
Itikio la tatizo linaweza kunisaidia vipi?
Mfanyakazi wa tatizo anaweza kutathmini kinachofanyika, kutuliza tatizo na kuunda mpango wa kumweka kila mtu salama. Pia, wanaweza kukuunganisha na rasilimali zingine za kijamii ili kukusaidia na mahitaji na usaidizi unaoendelea.
Nini kitafanyika nikipiga simu?
Mfanyakazi wa tatizo la afya ya akili atajibu simu hiyo na kukuomba umweleze kinachotendeka. Kwanza, watakuuliza maswali ili wajue ikiwa wewe au mtu unayemjali yuko kwenye hatari. Watachukua maelezo fulani ya kimsingi na kusikiza mahitaji yako. Kisha, watakusaidia kufikiria kuhusu machaguo yako ya kushughulikia tatizo hilo. Hii inaweza kujumuisha mtu kukutembelea katika eneo ulilochagua.
Nitaongea na nani?
Mfanyakazi wa tatizo aliyefunzwa kuhusu afya ya akili.
Washiriki wa timu ya kushughulikia tatizo wana hati au sifa gani?
Hawa ni wataalam na watendaji wa afya ya akili. Uwanja wao wa kazi unaweza kuhusu kazi za kijamii, saikolojia, ndoa na tiba ya familia, ushauri nasaha au uuguzi. Baadhi ya timu pia zina Wataalam wa Rika Moja wa Familia Waliothibitishwa.
Itachukua muda gani kupata usaidizi?
Simu ina wafanyakazi 24/7 (wakati wote). Ukiamua kwamba ungependa mfanyakazi wa tatizo akutane nawe ana kwa ana, watakuja haraka iwezekanavyo siku hiyo.
Je, hii itanigharimu chochote?
Hutagharamia chochote kutoka kwenye mfuko wako. Ikiwa bima yako inalipia huduma kama hii, tutawapa bili hii tukikutembelea sisi wenyewe.
Je, ikiwa sina bima?
Hauhitaji bima ili upate huduma hii.
Je, hii itawekwa siri? Je, utaambia mtu kwamba nilipiga simu?
Simu hii ni ya siri (ya kibinafsi). Hata hivyo, ikiwa mtu yuko katika hatari kubwa ya kujiumiza au kuumiza wengine, mfanyakazi wa tatizo huenda ahitaji kuchukua hatua ili kuhakikishia usalama wa kila mtu.
Mimi ni mtu mzima anayejali na nina wasiwasi kuhusu kijana fulani. Je, ni lazima nimpate mwanafamilia au mlezi wake kabla nipige simu?
Unaweza kupigia timu simu kwa usaidizi hata kama mlezi hayuko. Watazungumza nawe kuhusu hali hiyo na kukusaidia kuamua hatua zifaazo za kuchukua. Huwa inahitajika kwamba mzazi au mlezi wa mtoto awe kwenye mchakato, lakini kuna mambo yasiyofuata taratibu za kawaida.
Mimi ni kijana na nina tatizo. Je, nikiwapigia simu, ni lazima mpigie wazazi wangu?
Mfanyakazi wa tatizo atazungumza nawe ili ajue kinachotendeka na jinsi tunavyoweza kusaidia. Huwa tunataka wazazi wahusishwe, lakini kuna mambo yasiyofuata taratibu za kawaida.
Je, ninaweza kutuma ujumbe mfupi badala ya kupiga simu?
Kwa sasa, huduma ya ujumbe mfupi haipatikani kwa timu za tatizo zilizoko kwenye eneo la Twin Cities metro.
(in English)